Raphael
Warnock(51) wa Democratic amemshinda mgombea useneta wa Republican, Kelly
Loeffler na kuandika historia yakuwa Seneta wa kwanza mweusi wa Georgia, Jimbo
lililoundwa na urithi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Warnock
amepata ushindi wa asilimia 50.6 dhidi ya asilimia 49.4 za mgombea wa
Republican.
Warnock,
hajawahi kushikilia wadhifa wa kisiasa aliochaguliwa hapo awali.
Tangu 2005,
amekuwa mchungaji Mwandamizi wa Kanisa la Atlanta la Ebenezer Baptist, ambapo,
Martin Luther King Jr alikulia kama mshiriki na baadaye mhubiri.
Warnock
anajulikana kwa kufanya kampeni dhidi ya adhabu ya kifo na usawa wa uchum na
kwa haki za uzazi za wanawake, haki za mageuzi ya polisi, na hatua juu ya shida
ya hali ya hewa.
Hili linakuwa ni pigo jingine kwa chama cha rais anayeondoka madarakani, Donald Trump.
EmoticonEmoticon