Rais wa
Marekani Donald Trump amesema kwamba hotuba yake ya wiki iliopita alipowataka
wafuasi wake kuvamia bunge la Congress 'ilistahili'.
Bwana Trump alisema kwamba ni upuuzi kwa wanachama wa
Democrarts kuweka juhudi za kumshataki bungeni kwa 'kuchochea uasi'.
''Nadhani
mchakato huo wa kunishtaki unasababisha hatari kubwa kwa taifa letu na
unasababisha hasira kubwa . Sitaki ghasia'' , bwana Trump alisema. ''Tutaenda katika jumba la bunge ili
kuwapongeza maseneta na wabunge wetu kwa ujasiri wao na huenda baadhi yao
hatutawapongeza sana , kwasababu huwezi kulirudishu nyuma taifa letu kwa
udhaifu. Lazima uonyeshe uwezo wako'' aliwahutubia maelefu ya wafuasi wake .
Alisema kwamba makamu wa rais Mike Pence ni sharti awe na
ujasiri wa kufanya anachoweza kufanya , akidai bila msingi kwamba bwana Pence
alikuwa na uwezo wa kikatiba kubadilisha matokeo ambayo yalikuwa yakihesabiwa
bungeni siku hiyo.
''Najua kwamba kila mtu hapa ataelekea katika jumba la bunge
ili kuhakikisha kuwa sauti zetu zinasikika kwa njia ya amani , alisema Trump.
Anaondoka
afisini tarehe 20 Januari wakati ambapo rais mteule Joe Biden ataapishwa.
Bunge la uwakilishi linatarajiwa kupigia kura kifungu cha sheria kuhusu kumshtaki rais huyo siku ya Jumtano.
EmoticonEmoticon