Tume ya
Mawasiliano ya Uganda (UCC) Jumanne iliagiza makampuni yanayotoa huduma ya
internet kufunga mitandao ya kijamii na app zote za mawasiliano siku mbili tu
kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini humo.
Mkurugenzi mkuu wa UCC, Irene Sewankambo, aliyaandikia barua
makampuni hayo, na kuyataka “kuhakikisha kwamba huduma ya mitandao ya kijamii
imesitishwa.”
Kufuatia agizo hilo, watumiaji wa mitandao ya kijamii
wameripoti visa vya kutoweza kuingia kwenye mitandao kama vile Facebook na
Twitter, kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda.
Mitandao mingine ni kama vile Viper, Whatsapp na Signal.
Vyombo vya habari nchini Uganda viliripoti Jumanne kwamba raia wengi walikuwa wanajaribu kutumia njia mbadala za VPN ili kuwasiliana kupitia baadhi ya App za mawasiliano.
EmoticonEmoticon