Tuzo za
Grammy za mwaka 2021 hazitafanyika tena mwezi huu huko Los Angeles Crlifornia
na badala yake zitatangazwa mwezi Machi kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya
virusi vya corona na vifo.
Waandaji wa
tuzo hizo waliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne kuwa onyesho la kila
mwaka litasogezwa mbele kutoka tarehe yake ya awali ya Januari 31 hadi tarehe
isiyojulikana mnamo mwezi Machi.
Tuzo hizo za Grammy zitafanyika Los Angeles katika Kituo cha Staples, Kaunti ya Los Angeles, ambako ndio kitovu cha ugonjwa huko California, ambako umezidi vifo 10,000 na imekuwa na asilimia 40 ya vifo . Beyonce ndiye anayeongoza katika tuzo hizo mwaka huu akiwa na uteuzi katika vitengo tisa.
EmoticonEmoticon