Akaunti za
Twitter na Facebook za rais wa Marekani Donald Trump zimefutwa kwa muda baada
ya kutuma ujumbe kwa wafuasi wake waliovamia bunge la Marekani.
Katika ujumbe uliotumwa katika
mitadao hiyo kwa waandamanaji, alisema:‘Nawapenda’ akiwataka kwenda nyumbani.
Pia alizungumzia kuhusu madai ya
uongo kuhusu udanganyifu uliofanyika katika uchaguzi huo.
Twitter ilisema kwamba inahitaji
kuondolewa kwa jumbe tatu za twitter za rais huyokwa kukiuka maadili.
Kampuni hiyo ilisema kwamba akaunti
ya rais huyo itasalia kufungwa kabisa iwapo jumbe hizo za twitter
hazitaondolewa.
Iliendelea kusema ukiukaji wa sheria
za twitter siku zijazo utasababisha kufutiliwa mbali kwa akaunti ya
@realDonaldTrump account".
Hatua hiyo ina maana kwamba siku za
Donald Trump katika mtandao wa twitter zitakuwa hatarini.
Rais huyo hajulikani kwa kuheshimu
masharti ya muongozo wa twitter kuhusu jamii. Wakati huohuo facebook ilimfuta
bwana Trump kwa saa 24 . Youtube pia iliondoa video hiyo.
Facebook ilisema: Tuliiondoa
kwasababu tuliamini kwamba inachochea badala ya kupunguza ghasia zilizokuwa
zikiendelea.
Wafuasi wake walivamia kiti cha
serikali ya marekanina kukabiliana na maafisa wa polisikitu kilichosababisha
kifo cha mwanamke mmoja.
Ghasia hizozilisitisha mjadala kuhusu
ushindi wa rais mteule Joe Biden.
Kabla ya ghasia hizo rais Trump
aliwaambia wafuasi wake mjini Washington kwamba uchaguzi huo uliibwa.
Saa chache baadaye ghasia kuzuka
ndani na nje ya jumba la Capitol Hill , alionekana katika video akirejelea
madai hayo ya uongo.
You tube ilisema kwamba iliiondoa
kanda hiyo ya video kwasababu ilikiuka seraza kusambaza madai ya udanganyifu
kuhusu uchaguzi uliopita.
Awali twitter haikuwa imeiondoa video
hiyo , na badala yake kuondoa uwezo wake wa kujibiwa , kupendwa na kutolewa
maoni.
lakini baadaye iliiondoa na kufuta akunti ya rais huyo anayeondoka madarakani.
EmoticonEmoticon