Uingereza
iliacha kufuata sheria ya EU saa 23:00 GMT, baada ya mpango mbadala wa usafiri
, biashara, uhamiaji na ushirikiano wa kiusalama kuanza kutekelezwa.
Boris Johnson alisema Uingereza ina " uhuru mikononi
mwake" na uwezo wa kufanya vitu "Tofauti na bora" na sasa muda
uliokuwa ukisubiriwa umekwisha .
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Uingereza itasalia
kuwa "rafiki na mshirika".
Mawaziri wa Uingereza wameonya kutashuhudiwa changamoto
katika siku na wiki chache zijazo, wakati sheria mpya zitakapoanza kutekelezwa
na mashirika ya Uingereza yanayofanya biashara na bara Ulaya yatakapoanza
kukumbana na mabadiliko hayo.
Maafisa
wamesisitiza mifumo mipya ya mipakani ''iko tayari'' kuanza kazi licha ya hofu
ya mizigo kukwama bandarini.
Uingereza ilijiondoa katika muungano huo wa kisiasa na kiuchumi uliyo na nchi wanachama 27 miaka mitatu na nusu iliyopita baada ya raia wa Uingereza kupiga kura ya maoni mwaka 2016, maarufu Brexit.
EmoticonEmoticon