Watu wengi
ambao wamewahi kupata ugonjwa wa virusi vya corona miili yao imejikinga yenyewe
na hawawezi kupata tena ugonjwa huo kwa karibu miezi mitano, utafiti
ulioongozwa na wizara ya Afya nchini Uingereza imeonesha.
Kama mwili uliwahi kupata maambukizi, asilimia ya kupata
maambukizi hayo yanapungua kwa 83 ikilinganishwa na wale ambao hawajawahi kupata
maambukizi hayo, wanasayani wamebaini.
Lakini wataalamu wameonya kuwa baadhi ya watu wanapata
maambukizi ya virusi vya corona tena na pia wanaweza kuambukiza wengine.
Maafisa wanasisitiza kuwa watu wanastahili kufuata sheria za kubaki nyumbani - ama wawe wamewahi kupata maambukizi au la.
EmoticonEmoticon