Hali ya
usalama imeimarishwa kuliko ilivyo kawaida katika mji mkuu wa Washington kabla
ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden hapo Januari 20.
Maafisa wa usalama na wale wa jiji hili kuu, wanatekeleza
hatua za usalama ambazo hazijawahi kutekelezwa ili kuepusha vurugu kama
iliotokea wiki iliyopita pale maelfu ya wafuasi wa Rais Trump walipovamia
majengo ya Bunge la Marekani.
Idara za usalama za Marekani zinazo simamia usalama wa
maandalizi ya sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule Joe Biden wana dhamira ya
kuepusha kutokea tena tukio lililoshuhudiwa wiki iliyopita katika majengo ya
bunge ambako watu watano walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Maelfu ya maafisa wa kikosi cha ulinzi wa taifa kutoka
majimbo kadhaa wanaletwa hapa Washington kuanzia mwisho wa wiki hii. Meya wa
jiji hili Muriel Bowser anasema kwamba sherehe za kuapishwa Biden zinazusha
changamoto ambazo hazijawahi kutokea kuanzia janga la COVID-19 hadi vitisho vya
wafuasi wa itikadi kali.
Bowser anasema : "Watu wanaokuja kuandamana kwa njia za
amani ni tofauti kabisa na wale watu tuliowaona wakivamia majengo ya bunge wiki
hii. Na nina dhani itabainika kwamba watu hao waliovamia bunge waliandaliwa na
kupata mafunzo.
Kupambana na ugaidi wa ndani ya nchi kunazusha changamoto za
kipekee za kisheria anasema Said Javed Ali mtaalamu wa masuala ya kupambana na
ugaidi katika chuo kikuu cha Michgan.
Ali anasema : "Unakabiliana na Wamarekani waliozaliwa na kukulia hapa nchini wenye haki za kulindwa chini ya katiba. Na wanafahamu mahala mipaka hiyo inapoanza na kumalizika kuhusiana na hadi kiwango gani cha harakati zao wanaweza kufanya kabla ya kugeuka kuwa uhalifu."
EmoticonEmoticon