Video Ya Polisi Imeonyesha Wakimfwatulia Mtu Mweusi Risasi (VIDEO)

Polisi huko Minneapolis wametoa video inayoonesha mauaji ya mtu mweusi yaliyotekelezwa na polisi. 

Mwathirika kijana mweusi, Dolal Idd, 23, alikuwa mshukiwa wa uhalifu na alisimamishwa na maafisa wa polisi Jumatano.

Walioshuhudia mauaji hayo wanasema, bwana Idd ndiye aliyeanza kufyatua risasi kabla ya polisi kujibu.

Video ya mauaji ya hivi sasa ya ufyatuaji wa risasi unaomhusisha afisa wa polisi ilitolewa Alhamisi. Abiria wa kike aliyekuwa kwenye gari na Bwana Idd amepata majeraha na pia hakuna polisi aliyejeruhiwa.

Mkuu wa polisi wa Minneapolis Medaria Arradondo amesema bunduki ilipatikana kwenye eneo la tukio.

"Nilipotazama video ambayo kila mmoja anaitazama - na uhalisia wa mambo - inaonekana aliyekuwa kwenye gari ndiye aliyeanza kufyatulia polisi risasi," amesema.

Watu ikiwemo baba yake Idd, Bayle Gelle walikusanyika kwenye eneo la tukio siku iliyofuata, na kusababisha hofu ya kuanza tena kwa maandamano.

"Alikuwa tu ameketi ndani ya gari, na akaanza kufyatuliwa risasi bila sababu yoyote, alisema kama alivyonukuliwa na shirika la habari la CBS News.

"Kwanini tumefika hapa?... Kwasababu ya ubaguzi wa rangi. Ni mwanaume mweusi. Tunataka kujua kwanini kijana wangu alipigwa risasi na kuuawa."

Meya wa mji huo Jacob Frey alisema amejitolea kuhakikisha anafahahamu kwa undani kilichotokea na kuwa haki itatende

"Tunajua maisha ya mtu yamekatizwa usiku huu na ule uaminifu kati ya jamii za watu weusi na maafisa wa polisi umezorota," amesema hivyo katika taarifa yake aliyotoa.

"Kujenga tena uaminifu uliokuwepo kutategemea na uwazi tu." 


EmoticonEmoticon