Waziri Mkuu
wa Uingereza Boris Johnson amesema utafiti wa awali unaonyesha kuwa virusi
vipya vya ugonjwa wa corona vilivyojitokeza Uingereza ndio hatari zaidi.
Data hiyo
imetokana na kulinganishwa kwa idadi ya vifo kati ya watu waliopata maambukizi
na virusi vipya ama vile vya zamani vya corona,maambukizi yanayosababishwa na
virusi vipya tayari yamesambaa kote Uingereza.
Johnson
amesema katika taarifa: kuwa mbali na kwamba vinasambaa kwa haraka, sasa hivi
pia inaonekana kwamba kuna ushahidi kuwa virusi vipya vile ambavyo mara
ya kwanza kabisa vimebainika London na kusini mashariki – huenda vikasababishwa
vifo vya watu wengi.
“Athari
kubwa imetokana na virusi hivyo vipya na hilo linamaanisha wizara ya afya sasa
hivi inakumbana na shinikizo kubwa.”
Kundi
lililokuwa linafanya utafiti, limehitimisha kuwa “kuna uwezekano mkubwa” virusi
hivyo vimekuwa hatari mno.
“Nataka
kusisitiza kuwa bado kuna sintofahamu kuhusiana na idadi na juhudi zaidi
zinahitajika lakini bila shaka inatia wasiwasi kwamba virusi hivyo vimechangia
ongezeko la idadi ya vifo pamoja na kiwango chake cha maambukizi.”amesema
Boris.
Uchunguzi wa
awali umeonesha kuwa virusi vipya vinasambaa kwa asilimia 30 na 70 haraka zaidi
ya virusi vyingine na inasemekana kuwa ni hatari zaidi kwa asilimia 30.
Virusi hivyo vipya mara ya kwanza vimebainika Kent mnamo mwezi Septemba na sasa hivi vinapatikana kwa nchi nyingi na maeneo ya England na Ireland Kaskazini.
EmoticonEmoticon