Wabunge
kadhaa wa Marekani hivi karibuni wamepokea vitisho kwa maisha yao, wakati
Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi akitaka usalama
uimarishwe katika Bunge la Marekani na kudai kuwa kuna hatari inayokuja
siyo tu kutoka uraiani lakini kutoka kwa “adui wa ndani” ya Bunge lenyewe.
Madai ya Pelosi Alhamisi yameonyesha kuongezeka kwa mvutano
kati ya vyama vya siasa Bungeni juu ya tishio la usalama tangu uvamizi wa mwezi
huu ndani ya Bunge uliofanywa na wafuasi wa Rais wa zamani Donald Trump, watu
watano waliuawa kufuatia ghasia hizo.
Zaidi ya
wabunge 30 walisaini barua wiki hii iliyotaka wapatiwe ulinzi zaidi katika
wilaya zao. Walieleza kuwa vitisho dhidi ya wabunge vimeongezeka sana katika
miaka ya karibuni, na takriban vitisho 4,900 vilitolewa katika mwisho wa mwaka
wa fedha unaoishia Septemba 2018. Ukilinganisha na vitisho zaidi ya 900
vilivyotolewa mwaka 2016.
Polisi katika
Bunge la Marekani wanasema wanachukua hatua kuwalinda wabunge wanapokwenda na
kutoka kazini, kwa mujibu wa barua pepe ya Afisa Mkuu wa Polisi Bungeni ambayo
shirika la habari la The Associated Press iliipata.
Timothy P.
Blodgett, kaimu askari msimamizi wa bungeni, ameandika katika barua pepe kuwa
jeshi la polisi linaweka mawasiliano maalum na wabunge, na pia amewasihi
kuripoti vitisho au vitendo vinavyotia shaka, wanaweza kuwafahamisha mipango
yao ya kusafiri.
Amesema Polisi wa Bunge watawekwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na kituo cha Treni cha Union mjini Washington katika siku zenye shughuli nyingi, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
EmoticonEmoticon