Wachunguzi Wa Corona Wa WHO Wazuiliwa Kuingia China

 

Maafisa wawili tayari walikuwa safarini kuelekea China, huku WHO ikisema tatizo ni ukosefu wa kuidhinshwa kwa visa.

Hata hivyo, China imepinga madai hayo, ikisema kuwa maelezo kuhusu ziara hiyo ikiwa ni pamoja tarehe, bado inapangwa.

Uchunguzi huo ulikuwa ufanyike baada ya Beijing kuitikia ombi la miezi kadhaa kutoka WHO.

Virusi vya corona viligunduliwa kwanza Wuhan mwisho wa mwaka 2019, mlipuko wa kwanza ukihusishwa na soko la nyama katika eneo hilo mji huo.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa "amesikitika sana " kwamba China haijakamilisha idhini ya maafisa hao kuingia nchini humo "ikizingatiwa kuwa maafisa wawili tayari wameanza safari na wengine walishindwa kusafiri dakika za mwisho".

"Nilihakikishiwa kwamba China inaharakisha kukamilisha mchakato wa ndani kwa maafisa hao," aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva siku ya Jumanne, akielezea kwamba amekuwa akiwasiliana na maofisa wa ngazi ya juu wa China akisisitiza kuwa "mpango huo ni muhimu kwa WHO na ulimwengu kwa ujumla".


EmoticonEmoticon