Waziri Mkuu
wa Niger amesema watu 100 wameuawa kwenye mashambulizi ya Jumamosi
yaliotekelezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Wajihad katika vijiji
viwili.
Brigi Rafini amesema watu 70 waliuawa katika kijiji cha
Tchombangou huku wengine 30 wakiuawa katika kijiji cha Zaroumdareye - vyote
vikiwa karibu na mpaka na Mali.
Hilo ni moja ya shambulizi baya zaidi kutokea wakati ambapo
nchi hiyo inaendelea kupambana na vita vya kikabila na wanamgambo wa Kiislamu.
Hadi kufikia sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na
mauaji hayo. Kulingana na meya wa eneo Almou Hassane, waliohusika walisafiri
kwa kutumia pikipiki 100," kulingana na shrika la habari la AFP
Inasemekana
kwamba wanamgambo hao waligawanyana katika makundi mawili na kutekeleza
mashambulizi hayo kwa wakati mmoja.
Aliyekuwa waziri Issoufou Issaka ameliambia shirika la AFP
kwamba wapiganaji wa jihadi walitekeleza mashambulizi hayo baada ya wanavijiji
kuwaua wanachama wao wawili ingawa hiilo halijathibitishwa rasmi.
Meya Hassane amesema baada ya mashambulizi hayo wanavijiji 75
waliachwa wakiwa na majeraha huku wengine wakipelekwa kupata matibabu katika
eneo la Ouallam mji mkuu wa Niamey.
Waziri Mkuu Rafini alitembelea vijiji hivyo Jumapili.
"Hali ni mbaya... lakini uchunguzi utafanywa ili waliohusika waweze kukabiliwa kisheria," amewaambia wanahabari.
EmoticonEmoticon