Wapinzani wa
Rais wa Marekani Donald Trump katika mabunge yote mawili wametoa wito wa rais
huyo kuondolewa madarakani baada ya wafuasi wake waliokuwa wakifanya vurugu
kuvamia bunge.
Seneta wa Democratic Chuck Schumer amesea Bwana Trump
anastahili kuondolewa mara moja. Na ikiwa sio hivyo, Spika wa bunge la
Wawakilishi Nancy Pelosi amesema anaweza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani
naye.
Kuondolewa kwa rais huyo kupitiamuswada wa kutokuwa na imani
naye, kutahitaji kuungwa mkono na wabunge wa Republican ambao kufikia sasa ni
wachache tu wanaoonekana kutofautiana naye.
Katika hotuba iliotumwa kwa njia ya video, Bwana Trump
alisema amejitolea kukabidhi mamlaka kwa amani.
Rais huyo
alisema utawala mpya utaapishwa Januari 20 na kutoa wito wa
"maridhiano".
Pia alisema, "hasira imesababishwa na vurugu, uasi wa
sheria na ghasia" zilizotokea Jumatano na kwamba "hasira lazima
zitulizwe". Video hiyo ilishirikishwa kwenye akaunti yake ya Twitter,
ambayo iliwezeshwa tena kutumika kuanzia Alhamisi baada ya kufungwa kwa muda
kwasababu ya tukio la uvamizi wa bunge.
Watu wanne walifariki dunia wakati wa uvamizi huo huku wengine 68 wakiwa wamejeruhiwa.
EmoticonEmoticon