China
inasema timu ya wanasayansi kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni itawasili wiki
hii huko Wuhan kuanza uchunguzi wake wa asili ya janga la virusi vya corona.
Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya nje Zhao Lijian alisema Jumanne kwamba timu hiyo ya
washiriki 10 itaondoka kutoka Singapore Alhamisi hii na kuruka moja kwa moja
kuelekea Wuhan, jiji la kati ambalo virusi vya corona iligunduliwa kwa mara ya
kwanza mwishoni mwa 2019.
Hatimaye
virusi vilienea karibu kila kona ya ulimwengu, na kusababisha vifo vya zaidi ya
milioni 1.9 kati ya karibu maambukizo milioni 91.
China imetaka
kubadilisha hadithi juu ya asili ya virusi, huku maafisa wakishinikiza nadharia
ugonjwa uliibuka kwanza katika taifa jingine.
Daktari Mike Ryan, mkuu wa mpango wa dharura wa WHO, aliwaambia waandishi wa habari huko Geneva Jumatatu kwamba shirika hilo "linatafuta majibu hapa ambayo yanaweza kutuokoa katika siku zijazo. Sio wakosaji na wala sio watu wa kulaumiwa.
EmoticonEmoticon