Watoto kumi
wachanga waliokuwa wametoka tu kuzaliwa wamefariki dunia katika hospitali moja
huko nchini India.
Wahudumu wa afya walijitahidi kuwahamishia eneo salama baada
ya kutokea kwa moto majira ya asubuhi.
Watoto wachanga saba wameokolewa kabla ya wazima moto
kuwasili katika hospitali hiyo ya Bhandara magharibi mwa jimbo la Maharashtra.
Waziri Mkuu Narendra Modi ameelezea tukio hilo kama
linalouumiza moyo.
Sababu ya
kutokea kwa moto huo bado haijulikani na uchunguzi unaendelea.
Moto huo ulianza takriban saa nane usiku, kulingana na
maafisa wa hospitali.
Juhudi za uokozi zilizuiwa na milipuko ambayo ilikuwa
inaendelea ndani ya wadi hiyo, kulingana na vyombo vya habari vya eneo.
Muuguzi mmoja aliyekuwa kazini alisema alifahamisha mamlaka
kuhusu tukio hilo baada ya kuona moshi unafuka.
"Mamlaka ya hospitali imenusuru watoto saba lakini 10
wamefariki dunia katika ajali hiyo ya kusikitisha," Daktari Pramod
Khandate amezungumza na wanahabari.
Katika ujumbe wa Twitter, Bwana Modi ametuma risala zake za
rambirambi kwa familia.
Waziri wa
masuala ya ndani wa India, Amit Shah, amesema "machungu aliyonayo
hayaelezeki" juu ya "hasara iliyotokea ambayo haiwezi
kurekebishika".
Aidha, waziri wa ulinzi Rajnath Singh amesema
"amehuzunishwa mno" na taarifa za vifo hivyo, na kuongeza kuwa:
"Salamu zangu za rambirambi ni kwa familia."
Bhandara ipo kilomita 62 kutoka kaskazini magharibi mwa eneo la Nagpur - moja ya miji mikubwa Maharashtra.
EmoticonEmoticon