Waziri Mkuu Wa Congo Atakiwa Kujiuzulu Ndani Ya Saa 24

 

Wabunge nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepiga kura kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilukamba.

Bwana Ilukamba, ambaye hakuwepo wakati wa kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa bungeni, amepewa saa 24 kujiuzulu.

Wabunge wanamshutumu Bw. Ilukamba, mshirika wa rais wa zamani Joseph Kabila, na mawaziri wake kwa utendaji kazi mbovu.

Kuanguka kwa serikali kunafungua milango kwa Rais FĂ©lix Tshisekedi kuteua mawaziri watiifu kwake.

Mwezi uliopita, Rais Tshisekedi aliuvunja muungano ulioundwa na mtangulizi wake, umoja ambao mawaziri washirika wake walitawala kwenye baraza la mawaziri.

Tangu wakati huo, Bw. Tshisekedi amekuwa akiwashawishi wabunge kuachana na muungano wa Bw Kabila, ambao hapo awali ulishikilia wengi bungeni, ukikwamisha mpango wa rais wa mageuzi.

Hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza nchini DRC katika historia ya miaka 60, serikali ikilazimishwa kujiuzulu.


EmoticonEmoticon