Waziri Wa Elimu Marekani Ajiuzulu Kufuatia Ghasia Za Washington

 

Waziri wa Elimu wa Marekani Betsy DeVos ametangaza kujiuzulu baada ya ghasia zilizotokea mjini Washington Jumatano, pale wafuasi wa Rais Donald Trump walipovamia bunge la nchi hiyo. 

Katika barua yake ya kujiuzulu aliyomtumia Trump, DeVos amesema uamuzi wake umetokana na matamshi anayopenda kuyatumia kiongozi huyo. Wanasiasa wengi wa chama cha Democratic wanaamini Trump kwa makusudi alichochea kutokea kwa fujo hizo. 

Wengine waliojiuzulu kwa sababu hiyo hiyo ni Waziri wa Usafiri, Elaine Chao, ambaye pia ni mke wa kiongozi wa maseneta wa chama cha Republican, Mitch McConnell, na kiongozi wa zamani wa utumishi ofisi ya Rais Trump na mjumbe maalumu wa Marekani huko Ireland Kaskazini, Mick Mulvaney.


EmoticonEmoticon