Jeshi la
Ethiopia limetangaza kwamba limemuua waziri wa zamani wa mambo ya nje Seyoum
Mesfin, mmoja wa wanachama waanzilishi wa chama Tigray People’s Liberation
Front (TPLF).
Bw.Seyum, ambaye alihudumu kama
waziri wa mambo ya nje wa kutoka mwaka 1991 hadi 2010, aliuawa pamoja na
wanachama wengine wa ngazi ya juu TPLF kaskazini mwa jimbo la Tigray, wanajeshi
walisema.
Serikali ilikuwa imetoa waranti ya
kukamatwa kwake- pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya juu katika chama hicho
– kufuatia oparesheni ya kijeshi ya mwezi Novemba eneo la Tigray. Zawadi ya
birr milioni 10 sawa na ($254,000; £187,000) iliahidiwa kutolewa kwa wale
watakaotoa taarifa zitakazosidia kukamatwa kwao.
Jeshi linasema kwamba liliwaomba
wajisalimishe lakini wakakata kufanya hivyo. Makumi ya wancahama wengine wa
TPLF waliuawa na wengine kukamatwa katika oparesheni ya hivi punde, iliongeza
kusema.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliamuru oparesheni ya kijeshi dhidi ya jimbo la Tigray mnamo Novemba 4 na kuiondoa madarakani chama tawala, baada ya vikosi vyake kuvamia kambi ya majeshi ya serikali.
EmoticonEmoticon