WhatsApp
inawalazimisha watumiaji wake kukubali iwasilishe maelezo yao binafsi kwa
Facebook ikiwa wanataka kuendelea kutumia huduma hiyo.
Kampuni hilo inawaonya watumiaji kupitia taarifa zinazotolewa
kwenye simu zao zinazosema "unahitajika kuruhusu agizo hili ili kuendelea
kutumia WhatsApp" - au wafute akaunti zao.
Lakini Facebook, ambayo inamiliki WhatsApp, imesema watumiaji
wa mtandao huo waliyopo Ulaya na Uingereza hawataathiriwa na muongozo huo na
watahitajika kukubali masharti mapya.
Hatua hiyo imeungwa mkono na baadhi ya watu wakisema ni
ushindi kwa wasimamizi wa faragha wa EU.
Muda wa
mwisho wakukubali mabadiliko hayo mapya katika maeneo hayo ni Februari 8, na
baada ya hapo "utahitajika kukubali agizo hilo ili kuendelea kutumia
WhatsApp", kampuni hiyo ilisema katika taarifa zinazowasilishwa kwa
watumiaji.
Sehemu ya sera ya faragha ya kimataifa ya awali ambayo
ilikuwa inawasihi watumiaji kukubali maelezo yao kuwasilishwa kwa Facebook kwa
hiari katika siku 30 za kwanza imeondolewa baada ya mabadiliko haya mapya
kuanza kutekelezwa.
Badala ya katika maagizo ya hivi punde, watumiaji
wanaelekezwa sehemu ya kutafuta msaada mtandaoni "ikiwa wangelipendelea
kufuta akaunti zao".
Facebook haijajibu ombi la kutaka ifafanue kwa nini iliamua kufanya ghafla mabadiliko hayo.
EmoticonEmoticon