Huduma za
serikali nchini Zimbabwe zimeathiriwa pakubwa baada ya amri ya kufunga baadhi
ya shuguli za kawaida ili kupunguza mambukizi ya virusi vya corona wakati idadi
ya vifo iliongezeka nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, taifa hilo la kusini
mwa Afrika limefungiwa shuguli za kawaida tangu Januari, wakati wiki iliopita
serikali ikitoa amri kwamba asilimia 10 pekee ya wafanyakazi wa serikali wawe
ofisini ili kuzuia maambukizi.
Janga hilo limeathiri maafisa wa ngazi za juu serikalini
ambapo tayari mawaziri wanne wamekufa, watatu miongoni mwao wakifa katika
kipindi cha wiki mbili zilizopota. Ofisi nyingi za serikali zilionekana tupu
kuanzia Jumatatu, wakati maafisa wa dharura pekee wakibaki.
Kwenye ofisi za kutoa pasi za kusafiria, huduma za dharura
zinatolewa pekee kwa wale wanaoonyesha vibali vya kufanya kazi kwenye mataifa
ya nje. Kwenye ofisi ya wizara ya elimu, ni maafisa wa mitihani pekee waliobaki.
Zimbabwe yenye jumla idadi ya watu milioni 15 kufikia sasa imeshuhudia maambukizi 31,320 na vifo zaidi ya 1,000. Kuna wasi wasi kuwa huenda watu wa Zimbabwe wanaoishi Afrika kusini waliingia nchini na aina mpya ya virusi vya Covid, wakati wa kipindi cha siku kuu za mwisho wa mwaka.
EmoticonEmoticon