Zimbabwe Yasitisha Shughuli Na Kutangaza Lockdown

 

Serikali ya Zimbabwe imesitisha shughuli za maisha ya kawaida kote Nchini humo kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19, hatua inayowaweka katika hali ngumu Raia wake wanaotegemea ajira ya sekta isiyo rasmi itachukua siku 30.

Waziri wa afya Constantino Chiwenga amesema kumekuwa na ongezeko kubwa katika msimu huu wa sherehe ambalo liliongeza marudufu idadi ya maambukizi yaliyorekodiwa katika mwaka mzima.

Ni huduma muhimu pekee kama vile hospitali, maduka ya dawa na maduka ya jumla yatakayoendelea kufanya kazi kwa siku 30 zijazo, hali inayoongeza mbinyo kwa familia ambazo tayari zinasumbuliwa na umaskini huku taifa hilo likikabiliwa na mgogoro mkali wa kiuchumi, mfumuko wa bei na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira.


EmoticonEmoticon