Rais wa Afrika Kusini
Cyril Ramaphosa amelegeza masharti dhidi ya virusi vya corona ikiwa ni pamoja
na kuruhusu pombe kuanza kuuzwa tena.
Fukwe zitafunguliwa na
nyumba za ibada zitafunguliwa kwa kuruhusu idadi ndogo ya watu.
Tangazo hilo limekuja
wakati bwana Ramaphosa akifurahia ujio wa chanjo nchini mwake.
Dozi milioni moja za
chanjo ya AstraZeneca - zinaweza kubadilisha hali ilivyo ya Covid-19 nchini
humo.
Kwa barani Afrika, Afrika
Kusini inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya corona na vifo
vilivyotokana na Covid 19.
Tangu janga la corona
lianze, zaidi ya watu milioni 1.4 walipata maambukizi ya virusi vya corona na
vifo 44,164 vilivyotokana na janga hilo kwa mujibu wa utafiti wa chuo kikuu cha
Johns Hopkins.
Mataifa mengi yameiwekea vikwazo vya usafiri Afrika Kusini kwa kuweka marufuku kwa abiria kutoka taifa hilo kuingia nchini mwao ili kuzuia maambukizi ya wimbi jipya la virusi vya corona ambavyo vinadhaniwa kuwa vimeanzia nchini humo na vinavyoshukiwa kuwa sugu hata kwa chanjo iliyopo.
EmoticonEmoticon