Aung San Suu Kyi Huenda Akashtakiwa Na Utawala Wa Kijeshi

 

Imefahamika kwamba viongozi wa kijeshi waliochukuwa madaraka kwa nguvu nchini Myanmar wanapanga kumfungulia mashtaka ya uhaini kiongozi wa kiraia, Aung San Suu Kyi. 

Ripoti zilizochapishwa katika mitandao mbalimbali ya mitandao ya kijamii zinasema uongozi mpya wa kijeshi uliochukua madaraka kwa nguvu na kumkamata kiongozi wa kiraia, Aung San Suu Kyi, na viongozi wenzake wengine, unapanga kumshtaki mwanasiasa huyo kwa kosa la uhaini.


EmoticonEmoticon