Baba Mzazi Wa Nicki Minaj Afariki Dunia

 

Baba mzazi wa rapa Onika Tanya Maraj Maarufu kama Nicki Minaj, Mzee Robert Miraj mwenye umri wa miaka 64 amefariki dunia akiwa hospitalini alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia ajali ya gari huko New York,

Taarifa iliyotolewa na polisi wa kaunti ya Nassau imesema Robert Maraj aligongwa na gari alipokuwa akitembea kando ya barabara huko Long Island Ijumaa jioni, na alifariki dunia siku ya jumamosi, jitihada za kumtafuta dereva wa gari hilo aliyekimbia baada ya tukio hilo zinaendelea.

Mwakilishi wa Minaj alithibitisha kifo hicho kwa TMZ, ingawa Minaj hajatoa taarifa yoyote kwa umma juu ya kifo cha baba yake

Minaj, mwenye umri wa miaka 38, aliyezaliwa huko Trinidad na kukulia katika Jiji la New York, Marekani.

Kifo cha baba yake kinakuja miezi minne tu baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza na mumewe Kenneth Petty.


EmoticonEmoticon