Wizara ya
mambo ya nje ya Italia imesema kuwa balozi wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo ameuawa katika shambulio dhidi ya msafara wa magari ya Umoja wa
Mataifa mashariki mwa nchi hiyo.
Balozi Luca Attanasio na mwanajeshi
mmoja wa Italia wameuawa katika shambulio lililotokea karibu na mji wa
Kanyamahoro
Maafisa katika mbuga ya wanyama ya
Virunga wanasema shambulio hilo lilikuwa jaribio la utekaji nyara.
Makundi mengi yaliyojihami
yanaendesha harakati zake karibu na mbuga hiyo inayopakana na Rwanda na Uganda.
Walinzi wa mbuga hiyo wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na kuuawa na waasi.
EmoticonEmoticon