Chanjo Ya Ebola Yawasili Guinea

 

Ndege maalum iliyobeba shehena ya chanjo ya Ebola imewasili nchini Guinea usiku wa Jumatatu.

Dhoruba ya vumbi iliyokumba eneo la Sahara siku ya Jumapili ililazimisha ndege hiyo kuelekezwa Senegal, hali iliyochelewesha kutolewa kwa chanjo kwa siku moja.

Shughuli ya kutoa chanjo itaanza kufanyika katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, hivi leo.

Dozi 11,000 ya chanjo hiyo zitapelekwa mji wa Nzérékoré kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Watu watano wamefariki hivi karibuni kutokana na Ebola.

Huu ni mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huo hatari Afrika Magharibi tangu mwaka 2016.


EmoticonEmoticon