DR Congo Yazindua Kampeni Ya Chanjo Ya Ebola Butembo

 

Kampeni ya chanjo ya Ebola imeanzishwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwezi huu, Shirika la Afya Duniani - WHO limesema.

DR Congo imethibitisha visa vinne vya ugonjwa wa Ebola tangu kutangazwa kwa mlipuko mwingine wa virusi hivyo Februari 7 huko Butembo.

Wafanyakazi wa afya katika vituo vya afya ambako mgonjwa wa kwanza wa Ebola alitibiwa walikuwa wa kwanza kupata chanjo, WHO imesema.

Taarifa hizo zinawadia baada ya Guinea iliyopo Afrika Magharibi kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo.

Awali, mlipuko wa Ebola huko DR Congo ulitangazwa Juni 2020. Na ulikuwa umesababisha vifo vya watu 2,287 tangu Agosti mwaka 2018.


EmoticonEmoticon