Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa February 05

 

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa February 5, 2021

1. Mshambuliaji Lionel Messi, 33, hajafikia mkataba wowote na timu ya Paris St-Germain au Manchester City. Mkataba wake na Barcelona ambao bado unasifika unamalizika msimu huu lakini atasubiri hadi mwisho wa msimu kuamua ikiwa atasalia kwenye klabu hiyo au atahamia kwengineko. 

2. Kylian Mbappe anataka kujiunga na Real Madrid, amesema Jese Rodriguez, aliyekuwa mchezaji mwenzake huko Paris St-Germain. 

3. Winga wa Ukraine Marian Shved, 23, amekubali kwamba alifanya makosa kujiunga na Celtic badala ya Genk miaka miwili iliyopita. Shved sasa hivi yuko kwa mkopo Mechelen kutoka Celtic. 

4. West Ham inatarajiwa kutoa kitita kingine cha pesa kwa ajili ya mshambuliaji wa Sevilla raia wa Moroccan Youssef En-Nesyri, 23, msimu huu. 

5. Vilabu sita vya Ligi ya Primia huenda vikacheza katika Ligi ya Mabingwa kuanzia mwaka 2024 kuendelea. Mapendekezo ya Uefa yatawezesha timu kucheza mechi 10 za makundi kila moja huku kukiwa na uwezekano Ligi ya Europa ikapunguza idadi ya timu zitazoshiriki ligi hiyo.


EmoticonEmoticon