Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne February 2, 2021
1. AFC Wimbledon inafikiria
kumchukua Emma Hayes - kocha wa timu ya wanawake ya Women's Super League ya
Chelsea - kama kocha wa kwanza mwanamke katika timu ya soka ya kulipwa kwa
wanaume nchini Uingereza.
2. Liverpool ilikuwa na euro
milioni 23 kama dau lao wakati inamwania beki wa kati wa Croatia Duje
Caleta-Car, 24, kiwango kilichokataliwa na Marseille.
3. Manchester United haikufikiria
kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Roma na timu ya taifa ya Bosnia-Herzegovina
Edin Dzeko, 34, ambaye alikuwa mshambuliaji wa Manchester City, wakati wa
uhamisho mnamo mwezi Januari licha ya mapendekezo ya vyombo vya habari vya
Italia.
4. Kocha wa Real Madrid Zinedine
Zidane ni lazima ashinde Ligi ya Mabingwa ili awe na uhakika wa kuendelea kuwa
kocha wa timu hiyo.
5. Kuendelea kujiamini kwa Manchester City katika safu ya kiungo wa kati kumeiwezesha kumruhusu mlinzi wa Uingereza Taylor Harwood-Bellis, 19, kujiunga na Blackburn kwa mkopo.
EmoticonEmoticon