Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne February 9, 2021
1. Manchester City bado wanataka
kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 33, msimu huu wa joto lakini
wanajiandaa wakisubiri mpaka mwezi Machi au Aprili.
2. Mshambuliaji wa Inter Milan, Mbelgiji Romelu Lukaku, 27, na Muingereza anayekipiga Southampton Danny Ings,28, ni miongoni mwa wachezaji wanaotazamwa na Manchester City wakati huu ambapo klabu hiyo ikimtafuta mshambuliaji mpya. City itakabiliwa na ushindani wa Paris St-Germain katika kumnasa mshambuliaji Lukaku.
3. Manchester United imeweka wazi
kuwa inamlenga Ibrahima Konate wa RB Leipzig, mwenye miaka 21 kuwa beki wao wa
kati muhimu. Watapata upinzani kutoka kwa Liverpool na Chelsea.
4. Chelsea itamchukua David Alaba
ambaye mkataba wake ndani ya Bayern Munich unamalizika katika msimu wa joto -
ikiwa tu beki wa kushoto wa Austria, 28, atapunguza kiwango cha mshahara
anachotaka, kiasi cha pauni 400,000 kwa wiki.
5. Inter Miami inayomilikiwa na David Beckham inafikiria kumnasa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa West Brom Kieran Gibbs,31, kwa uhamisho wa bure msimu huu.
EmoticonEmoticon