Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu February 8

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu February 8, 2021

1. Kocha wa Tottenham Jose Mourinho anaamini kuwa ni jambo la kusubiri ''muda unaofaa'' linapokuja suala la mazungumzo kuhusu mkataba mpya kwa ajili ya mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min, ambaye mkataba wake na Spurs utakwisha mwaka 2023. 

2. Kujeruhiwa kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Mhispania Sergio Ramos kunaweza kusimamisha mazungumzo yake kuhusu mkataba mpya na Real Madrid mpaka atakapopona, makataba wa mchezaji huyo mwenye miaka 34 unamalizika majira ya joto. 

3. Kiungo wa kati Mfaransa Tanguy Ndombele, 24, amekubali kuwa ilibidi abadilike kama alitaka kufanikiwa akiwa na Tottenham katika ligi ya Primia.

4. Kocha wa AC Milan Stefano Pioli amesema ni ''sawa'' kwa mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovich ''kuendelea kucheza'' katika klabu hiyo ya Italia. Mkataba wa mchezaji huyo, 39 na klabu hiyo ya Serie A unakamilika msimu wa joto.

5. Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 24, hajafunga katika michezo ya ligi ya Primia lakini amesema, pamoja na kwamba hajafunga kwa ''muda mrefu'' ataendelea kucheza na ''magoli yatakuja''. 


EmoticonEmoticon