Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano February 10

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano February 10, 2021

1. AC Milan wanajiandaa kuanza mazungumzo na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 39, kuhusu mkataba mpya ambao utamfanya kuwa na klabu hiyo mpaka atakapofikisha miaka 41. 

2. Manchester United watasubiri mpaka mwishoni mwa msimu kabla ya kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na kocha Ole Gunnar Solskjaer, ambaye mkataba wake utakwisha mwishoni mwa 2021-22. 

3. Inter Miami inataka kuwasajili wachezaji wawili wa zamani wa timu ya taifa ya England Ryan Shawcross, 33, kutoka Stoke City na beki Kieran Gibbs, 31, wa West Brom.

4. Real Madrid wanapendelea kumsajili mlinzi wa kushoto wa Bayern Munich David Alaba, 28, huku Chelsea ikionesha kutokuwa tayari kutimiza takwa la mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki. 

5. Manchester City itaanza mazungumzo na John Stones 26, kuhusu mkataba msimu huu kwa kutambua jukumu la mlinzi huyo wa England.


EmoticonEmoticon