Tetesi Za Soka Ulaya Jumamosi February 13, 2021
1. Winga wa klabu ya Borussia
Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 20, amejihakikishia kuwa
tacheza klabu nyengine msimu ujao lakini kuna matumaini finyu juu ya miamba ya
Dortmund kumuuza kwa pauni milioni 100 ambazo walikuwa wakitaka Manchester
United wazitoe miezi sita iliyopita.
2. Kocha wa wa Liverpool Jurgen
Klopp pia anatarajiwa kujaribu kumsajili mshambuliaji wa Udinese na raia wa
Argentina Rodrigo de Paul, kwa dau la pauni milioni 30.
3. Arsenal wanaamini wanaweza
kumsahwishi mshambuliaji kinda wao Folarin Balogun, 19, kusaini mkataba mpya.
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa England unafikia ukomo mwishoni mwa msinu na
tayari kuna klabu kadhaa barani Ulaya zinazomnyatia.
4. Klabu za Ujerumani Bayer
Leverkusen na Stuttgart pamoja na Rennes ya Ufaransa ni baadhi ya timu
zinazomuwania Balogun.
5. Klabu ya Liverpool wanajiandaa na kuondoka kwa kiungo wao mkabaji, Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, na wanataka kumsajili kiungo wa Borussia Monchengladbach Florian Neuhaus, 23, kama mrithi wake.
EmoticonEmoticon