Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu February 22, 2021
1. Chelsea imeripotiwa kuanzisha
mazungumzo na Bayern Munich kuhusu mpango wa kumsajili beki wa Bayern Munich
Niklas Sule kwa dau la £25.9m.
2. Aliyekuwa mkufunzi wa Leicester
na Watford Nigel Pearson anakaribia kuchukua ukufunzi wa klabu ya Bristol City
baada ya mazungumzo na klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza.
3. Mshambuliaji wa Argentina Paulo
Dybala, 27, anatarajiwa kuanza mazungumzo mapya na Juventus katika kipindi cha
siku chache zijazo.
4. Crystal Palace inamchunguza
beki wa kati wa Juventus na Romania mwenye chini ya umri wa miaka 21 Radu Radu
Dragusin, 19, ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa Tottenham na Newcastle.
5. Liverpool huenda ikampeana kiungo wa kati wa Japan Takumi Minamino, 26, kwa mbadala wa winga wa Sevilla na Argentina Lucas Ocampos, 26.
EmoticonEmoticon