Iran imeanza
kutengeneza madini ya uranium, licha ya kuonywa na mataifa yenye nguvu duniani
kwamba ni uvunjaji mwingine wa mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015.
Wakaguzi wa Shirika la kimataifa la udhibiti wa nguvu za
atomi wamethibitisha uwepo wa gramu 3.6 (0.1oz) za madini hayo katika kiwanda
cha Isfahan wiki iliyopita.
Iran inasema inafanya utafiti na kutengeneza madini hayo kwa
lengo la kutengeneza mafuta kwa ajili ya utafiti wa mitambo.
Lakini chuma cha uranium kinaweza pia kutumika kutengenezea
bomu la nyuklia.
Iran inasisistiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani,
lakini imekiuka makubaliano kadhaa katika mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015
katika kipindi cha miaka miwli iliyopita.
Inasema inakiuka mkataba huo kujibu hatua ya Marekani
kuiwekea vikwazo vya kiuchumi ambavyo vilirejeshwa tena mwaka 2018 na aliyekuwa
rais wa Marekani wakati huo Donald Trump wakati alipovunja mkataba huo kwa
kujiondoa.
Mrithi wake, Joe Biden, anasema Iran lazima irejee katika
kuheshimu kikamilifu mkata wa nyuklia kabla ya kuondolewa vikwazo. Lakini
kiongozi wa ngazi ya juu zaidi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei anasema Marekani
lazima iondoe vikwazo kwanza.
China ya mkataba huo Iran ilikubali kutotengeneza uranium au kufanya utafiti na kutengeneza madini hayo kwa muda wa miaka 15.
EmoticonEmoticon