Raisi Wa Marekani Joe Biden Akuza Mahusiano Yake Na Canada

 

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa Canada na Marekani ni marafiki wa dhati, wakati Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akiuita urafiki wao kuwa "usiokuwa wa kawaida” Ijapokuwa vizuizi vya Covid-19 viliwatenganisha viongozi hao wawili kimwili, walifanya kila liwezekanalo kudhihirisha kuwa nchi hizo kubwa jirani zimerejesha ushirikiano wao wa tangu zamani baada ya mvutano wa sera za Trump za "Marekani Kwanza.” 

"Pia tumekubaliana kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu ili kuimarisha ugavi, usalama na uthabiti na kuhakikisha kuwa Canada na Marekani zinaendesha ufufuaji thabiti wa uchumi ambao utamnufaisha kila mtu, na sio tu wale walioko kileleni." Amesema Biden

Trudeau alimpongeza Biden – ambaye aliirejesha Marekani katika muafaka wa tabia nchi wa Paris wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu – kwa sera zake kuhusu suala la ongezeko la joto duniani. 

Waziri mkuu huyo, ambaye wakati mwingine alikuwa na mahusiano mabaya na Trump alieleza kuhusu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa nchi zao

"Tunapitia nyakati ngumu, bila shaka. Lakini hatuko peke yetu katika hali hiyo. Canada na Marekani ni washirika wa karibu, na muhimu zaidi, washirika wa kibiashara, na marafiki wa tangu zamani. 

Na tutaendelea kuungana ili kulishinda janga hili na kujenga mustakabali imara na najua urafiki wetu utakuwa imara hata zaidi." Amesema Trudeau.


EmoticonEmoticon