Kijiji
kimoja cha Indonesia kimekumbwa na mafuriko yenye rangi ya damu baada ya maji
kuingia katika kiwanda kimoja cha nguo.
Rangi iliokuwa ikitumika katika nguo ilisombwa na maji hayo
na kusafirishwa katika barabara za kijiji cha Jenngot katikati ya eneo la Java
siku ya Jumamosi.
Eneo hilo lililopo kusini mwa mji wa Pekalongan linasifika
kwa tamaduni yake ya viwanda vya kutia nguo rangi.
Maelefu ya watu mitandaoni waliasambaza picha za maji hayo yenye rangi katika kijiji hicho.
Afisa mmoja
wa shirika la misaada alithibitisha kuwa picha hizo zilikuwa za kweli.
''Mafuriko hayo ya rangi ya damu yanatokana na rangi za
kuweka katika nguo ambazo zilisombwa na mafuriko'', Dimas Arga Yudha aliambia
chombo cha habari cha Reauters.
''Itapotea baada ya kuchanganyika na maji ya mvua baada ya
muda''.
Mito katika
eneo la Pekalong imebadilisha rangi kutokana na rangi hiyo ya nguo huku mafuriko
ya rangi ya kijani yakikumba kijiji chengine mwezi uliopita , kulingana na
Reuters.
Indonesia mara kwa mara hukumbwa na mafuriko huku takriban
watu 43 wakifariki kutokana na kimbunga kilichopiga mji mkuu Jakarta mapema
mwaka huu.
Wakaazi walitumia ndege kumwagia kemikali mawingu ili kuzuia mvua huku mafuriko mabaya yakiripotiwa katika eneo hilo tangu 2013.
By Bbc
EmoticonEmoticon