Kiongozi Wa Myanmar Suu Kyi Akabiliwa Na Shtaka Jipya, Maandamano Yanaendelea

 

Kiongozi wa Myanmar ambaye yupo kizuizuni bi, Aung San Suu Kyi, ameongezewa shtaka la pili la jinai mahakamani alipofika kusikiliza kesi inayomkabili.

Bi Suu Kyi, ambaye hapo awali alishtakiwa kwa kumiliki kifaa cha mawasiliano aina ya redio sasa anadaiwa pia kukiuka Sheria ya Maafa ya Asili nchini humo.

Hata hivyo Jeshi la Myanmar hapo awali lilisema kuwa litatekeleza ahadi yake ya kufanya uchaguzi mpya na kuachia madaraka walioitwaa.

Huku hayo yakiendelea, waandamanaji wanaopinga mapinduzi hayo ya kijeshi wanadai kuachiliwa kwa viongozi wao waliowachagua kidemokrasia.

Katika mkutano wa kwanza wa wanahabari tangu kuangushwa kwa serikali, msemaji wa jeshi Brigedia Generali Zaw Min Tun amesema vikosi vya jeshi havitabaki madarakani kwa muda mrefu, na akaahidi "kurudisha nguvu kwa chama kilichoshinda" kufuatia uchaguzi uliopangwa. Hata hivyo tarehe ya uchaguzi mpya bado haijatajwa.


EmoticonEmoticon