Kiongozi Wa Zamani Wa Waasi Dominic Ongwen Akutwa Na Hatia Na Mahakama Ya ICC

 

Kiongozi wa zamani wa waasi Dominic Ongwen amekutwa na hatia kwa makosa ya uhalifu wa kivita katika Mahakama ya Kimataifa, ICC

Bw. Ongwen, kamanda anayeogopewa wa jeshi la Lord's Resistance (LRA) , ni mfuasi wa kwanza wa jeshi hilo kufikishwa katika mahakama hiyo.

Alikabiliwa na makosa 70 ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, lakini aliondolewa baadhi ya mashtaka

Mashtaka hayo yote yanahusu shambulio kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Uganda mnamo 2004.

Kesi hii ilisababisha mahakama kuwa katika njia panda kwani alionekana kuwa mwathiriwa na pia mhalifu.

Alisema kuwa alitekwa na LRA na kulazimishwa kuwa mwanajeshi akiwa mtoto, kabla ya kupanda akishika nafasi mbalimbali mpaka kuwa Naibu kamanda wa Joseph Kony.

Lakini akisoma uamuzi wake, jaji anayesimamia kesi hiyo Bertram Schmitt alisema: "Hatia yake imethibitishwa bila shaka yoyote."

Alihukumiwa kwa makosa kadhaa ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, mateso, utumwa wa kingono na uporaji.

ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwake mwaka 2005 na Marekani na vikosi vya Afrika wamekuwa wakimtafuta tangu mwaka 2011.

Mwaka 2014 alijisalimisha nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati na kesi yake iliyodumu kwa miaka mitatu na nusu huko Hague ilimalizika mwezi Machi.

Mawakili wake walikuwa wameomba aachiliwe na walinukuliwa na shirika la habari la Reuters wakisema katika hoja ya kuhitimisha"Wakati Ongwen alitekwa nyara hakuwa na cha kufanya, alifanywa mtumwa. Utumwa huo uliendelea hadi alipoondoka msituni."

Lakini waendesha mashtaka waliripotiwa wakisisitiza kuwa alikuwa mtu mzima wakati wa makosa hayo hivyo haiwezekani kutowajibishwa.


EmoticonEmoticon