Korea
Kaskazini imeshikwa ikijaribu kuiba teknolojia inayotumika kutengeneza chanjo
ya virusi vya corona kutoka kwa kampuni ya utengenezaji dawa ya Marekani
Pfizer, kulingana na maafisa wa kijasusi wa Korea Kusini.
Hadi kufikia sasa haijabainika ni taarifa gani hasa ambazo
zimeibwa.
Shirika la kijasusi la taifa la Korea Kusini limechukua hatua
binafsi na kutaarifu wabunge juu ya kinachodaiwa kuwa uvamizi, kulingana na
shirika la habari la eneo la Yonhap.
BBC imewasiliana na kampuni ya Pfizer ili kupata tamko lao
lakini hadi kufikia sasa bado haijasema lolote.
Korea
Kaskazini bado haijawahi kuripoti hata kisa kimoja cha maambukizi ya ugonjwa wa
virusi vya corona.
Hata hivyo, nchi hiyo inatarajiwa kupokea dozi milioni 2 za
chanjo ya AstraZeneca wiki chache zijazo.
Korea Kaskazini ilifunga mipaka yake mnamo mwezi Januari mwaka jana muda mfupi baada ya ugonjwa wa virusi cya corona kuanza kujitokeza nchini China.
EmoticonEmoticon