Mwanasiasa
mkongwe na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ),
Maalim Seif Sheriff Hamad (76), amefariki dunia.
Akihutubia Taifa kwa njia ya televisheni, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Mwinyi, alisema Maalim Seif
alifariki dunia akiwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete
iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa
takribani wiki mbili.
Maalim Seif amefariki dunia akiwa ametumikia wadhifa wa makamu wa kwanza wa rais wa SMZ kwa chini ya siku 100 - akiwa sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoundwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2020.
Kifo chake kinahitimisha safari ya
kisiasa ya mwanasiasa mashuhuri kuliko wote wa Zanzibar na kiongozi ambaye
alizibeba siasa za upinzani katika visiwa hivyo katika muda wa miaka 30
iliyopita.
EmoticonEmoticon