Madaktari huko New York wamefanikiwa upasuaji kupandikiza uso na mikono Joe DiMeo, 22, ambaye alifanyiwa upasuaji huo wa saa 23, uliofanywa na timu ya zaidi ya wahudumu wa afya 140 mwezi Agosti mwaka jana.
Ajali ya gari mwaka 2018 ilimwacha Bw DiMeo na majeraha ya kuungua kwa
kiwango cha zaidi ya 80% ya mwili wake. Vidole vyake vilikatwa na alipoteza
midomo na vigubiko vya macho.
Alisema operesheni hiyo ilimpa "nafasi ya pili maishani".
Bwana DiMeo alikuwa
akienda nyumbani kutoka zamu ya usiku alipolala kwenye usukani. Gari lake
lilianguka, likawaka moto.
Alikaa miezi minne katika kitengo kinachoshughulika na wagonjwa
walioungua moto, ambacho kilijumuisha wakati alipokuwa hana fahamu . Kisha
Bwana DiMeo alikuwa na upasuaji zaidi ya mara 20 wa kutengeneza mwili.
Mwaka 2019, alipelekwa kwenye kituo cha matibabu cha kitaaluma huko New
York, NYU Langone, ambapo alifanyiwa upasuaji wa upandikizaji mwezi Agosti
mwaka jana.
Eduardo Rodriguez, mkurugenzi wa Programu ya Kupandikiza Uso, alisema:
"Tulitaka kumpa sio tu operesheni ambayo ilimfanya aonekane bora, lakini
mwishowe ilibidi ifanye kazi vizuri, hasa mikono."
Bwana DiMeo alitumia siku 45 akiwa chini ya uangalizi baada ya upasuaji
na miezi miwili zaidi hospitalini, ambapo alilazimika kujifunza jinsi ya
kufungua vigubiko vya macho na kutumia mikono yake mipya.
Upandikizaji wa uso na mikono miwili uliwahi kufanyika hapo awali
lakini yote haikufanikiwa. Mgonjwa mmoja alikufa kutokana na changamoto na
mwingine mikono yake iliondolewa baada ya kushindwa kufanya kazi, hospitali
ilisema.
Bw Rodriguez anasema Bw DiMeo, ambaye hufanya hadi saa tano za
ukarabati kwa siku, ndiye "mgonjwa aliye na motisha zaidi" aliyewahi
kukutana naye.
"Anataka kufanya kazi kwenye michezo, anapenda kucheza gofu, na
anataka kurudi kwenye kozi. Ninavutiwa kila wakati na kiwango cha uzani ambao
anaweza kuinua
Bwana DiMeo anasema sasa anaweza kufanya mazoezi mwenyewe na
kutengeneza kifungua kinywa.
"Hii ni zawadi ya mara moja katika maisha, na natumaini familia inaweza kupata faraja kujua kuwa sehemu ya wafadhili inaishi na mimi," alisema. "Wazazi wangu na mimi tunashukuru sana kwamba nimepewa nafasi hii ya pili."
EmoticonEmoticon