Maelfu Wakusanyika Kwa Waandamana Kupinga Kufungwa Kwa Mpinzani Wa Putin Kote Urusi

 

Maelfu ya Warusi wameshiriki maandamano ambayo hayakuidhinishwa na mamlaka nchini Urusi kudai kuachiliwa huru kwa kiongozi wa upinzani aliyefungwa jela Alexei Navalny.

Zaidi ya watu 5,000 wamezuiliwa, kikundi kimoja kinachofuatilia matukio nchini humo kimesema.

Bwana Navalny alifungwa jela aliporejea nchini Urusi baada ya kupona jaribio la kumuua kwa sumu kwa kutumia kemikali inayoathiri neva.

Bwana Navalny amelaumu huduma za usalama kwa shambulio hilo lakini Kremlin imekanusha madai hayo.

The opposition figure was arrested after arriving in Moscow from Germany, where he spent months recovering from the near-fatal incident.

Mpinzani huyo wa serikali ya Urusi alitakamtwa baada ya kuwasili kutoka Ujerumani alipokuwa akipata matibabu kwa miezi kadhaa baada ya tukio hilo ambalo nusra limsababishie kifo.


EmoticonEmoticon