Mahakama Ya ICJ Kusikiliza Kesi Ya Iran Dhidi Ya Viwakzo Vya Marekani

 

Mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa imekubali kusikiliza malalamiko ya Iran ya kutaka iondolewe vikwazi ilivyowekewa tena na Marekani wakati wa utawala wa Donald Trump. 

Waziri wa kigeni wa Iran Mohammed Javad Zarif amepongeza uamuzi huo wa Jumatano unaohusu kesi iliyowasilishwa miaka mitatu iliyopita katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) mjini The Hague.

Iran inadai rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, alikiuka makubaliano ya urafiki ya mwaka 1955 kati ya nchi hizo mbili, alipojitoa kwenye makubaliano ya nyuklia. Na baadae Trump aliamrisha kuirudishia tena vikwazo vya kiuchumi Iran.

Marekani imesema mahakama ya ICJ ya mjini The Hague haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. 

Na imesisitiza kwamba vitendo vya Iran vinahatarisha usalama wa wa kimataifa. Hata hivyo majaji katika mahakama hiyo wameyakataa madai yote ya Marekani.

Rais wa ICJ Abdulqawi Ahmed Yusuf amesema mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza ombi lililowasilishwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ilijibu kwa kusema imesikitishwa sana na uamuzi huo.

Msemaji wa serikali ya Marekani Ned Price, amesema baadae watatoa maelezo zaidi juu ya kwanini madai ya Iran hayana maana.


EmoticonEmoticon