Mapigano Mapya Yameibuka Yemen Kati Ya Wahouthi Na Vikosi Vya Serikali

 

Waasi wanataka kupata udhibiti wa Marib, kufunga mpaka wa kusini wa Saudi Arabia na kuchukua udhibiti wa kisima cha mafuta katika jimbo hilo ambalo litawapa faida katika mazungumzo ya amani

Mapigano makali kati ya vikosi vya serikali inayotambuliwa kimataifa ya Yemen na waasi wa ki-Houthi yameibuka tena Jumapili na kuongeza wiki ya ghasia katika mkoa wa kimkakati wa Marib, nchini Yemen, maafisa wamesema. 

Huku darzeni ya watu wakiwa wameuwawa, mapigano haya yanatia shaka kubwa juu ya juhudi zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa za kuanzisha tena mazungumzo ya kumaliza miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Waasi wanaoungwa mkono na Iran, mapema mwezi huu walifanya tena shambulizi kwenye jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, ngome inayopinga wa-Houthi inayoshikiliwa na serikali inayotambuliwa kimataifa. 

Lakini walikabiliwa na upinzani mkali na hawajaweza kusonga mbele kufuatia idadi kubwa ya vifo kutoka kwa wa-Houthi, maafisa wa jeshi kutoka pande zote mbili wamesema.


EmoticonEmoticon