Shirika la Umoja wa Mataifa la afya, WHO hapo jana limeridhia chanjo dhidi ya virusi vya corona ya AstraZeneca kuanza kupelekwa kwenye mataifa masikini, baada ya kuithibitisha kwa dharura.
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya, WHO hapo jana limeridhia chanjo dhidi ya virusi vya corona ya AstraZeneca kuanza kupelekwa kwenye mataifa masikini, baada ya kuithibitisha kwa dharura.
Mataifa
ya kipato cha chini na cha kati yanatarajiwa kupata dozi ya kwanza ya chanjo
mwishoni mwa mwezi Februari ikiwa ni sehemu ya mpango wa kimataifa wa
mgawanyo wa chanjo, COVAX.
Shirika hilo
linataraji kupeleka dozi milioni 336 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka
na hadi bilioni 2 ifikapo mwishoni mwa mwezi Disemba.
Kulikuwa na matarajio kwamba mpango huo wa COVAX ungeanza sambamba na utoaji wa chanjo kwa mataifa tajiri.
Hata hivyo, miezi miwili baada ya mataifa hayo kuanza, hakuna chanjo hata moja iliyoanza kutolewa miongoni mwa watu bilioni 2.5 waliopo kwenye mataifa masikini zaidi yapatayo 130.
EmoticonEmoticon