Mawakili wa
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump wanasema wanahitaji siku moja tu
kuwasilisha kesi ya mteja wao ambaye anakabiliwa na mashtaka kwenye baraza
la Seneti la Marekani.
Mawakili wa Trump watatoa utetezi wa rais huyo wa zamani
Ijumaa bila ushahidi wowote wa moja kwa moja kutoka kwake kwani amekataa
kushiriki katika kesi hiyo.
Utetezi unafuatia siku mbili za uwasilishaji wa mashtaka
uliofanywa na Wademocrat katika Bunge wanaohusisha matamshi ya Trump kwenye
mkutano wa Januari 6 na vitendo vya genge la wafuasi wake waliovamia jengo la
bunge la Marekani muda mfupi baadaye katika jaribio la kuzuia urasmishaji wa
matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020.
Katika hatua isiyo ya kawaida Alhamisi, Maseneta watatu wa
Republican Lindsey Graham wa South Carolina, Ted Cruz wa Texas na Mike Lee wa
Utah ambao ni wasimamizi katika kesi hiyo, walikutana na mawakili wa Trump.
Kituo cha televisheni cha CNN kimeripoti kwamba David Schoen, mmoja wa mawakili wa Trump, alisema wabunge hao walitaka kuhakikisha kuwa timu ya utetezi ya Trump ilikuwa inajua utaratibu kabla ya uwasilishaji wa utetezi Ijumaa
EmoticonEmoticon