Mawakili Wasema Wafuasi Wa Trump Walivamia Bunge Kwa Hiari Yao

 

Mawakili wa Donald Trump wamejibu mashtaka dhidi yake, wakisema wafuasi wa rais huyo wa zamani wa Marekani walivamia Bunge huko Washington DC tarehe 6 mwezi Januari kwa hiari yao.

Kesi ya Bw Trump katika Seneti inatarajiwa kuanza Jumanne baada ya kushtakiwa kwa mara ya pili na Baraza la Wawakilishi mwezi uliopita.

Ameshtakiwa kwa "kuchochea vurugu" katika hotuba kwa wafuasi kabla ya vurugu kutolea. Bw Trump anasema hatatoa ushahidi.

Watu watano, pamoja na afisa wa polisi, walifariki wakati kundi la wafuasi wa Trump liliposhambulia jengo la Capitol, na kulazimu wanasiasa na wafanyakazi kujificha kwenye ofisi.

Bwana Trump ndiye rais pekee wa Marekani katika historia aliyewahi kushtakiwa mara mbili na mmoja kati ya watatu tu ambao walishtakiwa kabisa.

Katika muhtasari wa kabla ya kesi uliotolewa Jumatatu, mawakili wa rais huyo wa zamani walisema kwamba nyaraka za FBI zimeonesha kuwa maandamano hayo yalipangwa siku chache kabla, ikimaanisha kwamba Bw Trump hakuweza kuhimiza vurugu hizo.

Wanasisitiza pia kuwa kesi hiyo ni kinyume na katiba kwa sababu Bw Trump ameacha kazi na sasa ni raia.


EmoticonEmoticon