Mitandao Bado Imefungwa Huku Maelfu Wakiandamana Kupinga Mapinduzi Ya Jeshi Huko Myanmar

 

Maandamano makubwa yameshuhudiwa nchini Myanmar. Kundi kubwa la vijana limeingia barabarani kuupinga utawala mpya wa jeshi la nchi hiyo, licha ya kuzimwa kwa mitandao kote nchini kwa lengo la kuudhoofisha upinzani. 

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kwenye Twitter kwamba huduma za mitandao na mawasiliano lazima zirejeshwe kikamilifu kuhakikisha uhuru wa kujieleza na wa kupata habari. 

Mkuu wa sera ya umma ya mtandao wa Facebook kwa eneo la Asia-Pacific Rafael Frankel amesema kwenye taarifa yake kwamba katika wakati huu muhimu, watu wa Myanmar wanahitaji kupata habari na kuweza kuwasiliana na familia zao. 

Hata hivyo kuzimwa kwa mitandao hakukuwazuia maelfu ya waandamanaji hao kukusanyika katika jiji kuu la Myanmar, Yangon mnamo siku ya Jumamosi. 

Mikusanyiko ilianzia kwenye barabara iliyo karibu na Chuo Kikuu cha Yangon ambapo waandamanaji walipunga mikono kwa ishara ya vidole vitatu vya kati ambayo imekua ndio ishara ya kupinga uporaji wa madaraka uliofanywa na jeshi.

Kikosi kikubwa cha polisi wa kuzuia ghasia kilifunga barabara za karibu na maeno walipokusanyika waandamanji, na malori mawili ya maji ya kuwasha yakiwa yameegeshwa katika eneo hilo.


EmoticonEmoticon